Occupational Safety and Health Authority
  +255-22-2760548 / 2760552       info@osha.go.tz                     

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

About OSHA

OSHA ni Wakala wa serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu). Taasisi hii ina wajibu wa kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vilivyopo katika sehemu za kazi ambavyo vinaweza kusabisha magonjwa na ajali. Wajibu huu unatekelzwa kupitia usimamizi wa Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.

Historia ya OSHA inarudi nyuma hadi mwaka 2001 ambapo ndipo ilipoanzishwa chini ya Sheria Na. 30 ya Wakala wa Serikali ya mwaka 1997 kama sehemu ya Mpango wa Maboresho katika utoaji wa Huduma za Serikali kwa wananchi. Makusudi ya kuanzishwa kwa OSHA ni kupata chombo cha serikali kwa ajili ya kusimamia Usalama na Afya mahali pa kazi. 

OSHA ina jukumu la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira ambayo ni salama na yenye kulinda afya zao kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa katika kuzuia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

Taasisi hii ina majukumu makuu manne;

 • Kusimamia Utekelezaji wa Sheria Namba 5 ya mwaka 2003 ya Usalama na Afya na Mahali pa Kazi.
 • Kushauri serikali kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi, kuhusiana na sera, kanuni na miongozo mbalimbali ya usimamizi wa Usalama na Afya Nchini ikiwemo kushauri namna ya kuridhia mikataba ya kimataifa kuhusu masuala ya Usalama na Afya.
 • Kuongeza uelewa miongioni mwa wadau kususiana na masuala ya Usalama na Afya kwa kutoa mafunzo mbalimbali ikiwemo kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau
 • Kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na masuala ya usalama na afya katika sehemu za kazi ili kuweza kushauri serikali namna bora ya kutekeleza sheria tajwa.

Katika kutekeleza majukumu tajwa, Wakala hufanya shughuli mbali mbali kama ifuatavyo;

 1. Kusajili sehemu za kazi;
 2. Kufanya ukaguzi wa jumla (General Inspections); 
 3. Kufanya ukaguzi maalum (specific inspections) mfano ukaguzi wa usalama wa umeme; vyombo vya kanieneo (Pressure vessels) na ukaguzi wa vifaa vya kunyanyulia vitu vizito (Lifting appliances);
 4. Kutathmini hatari zilizopo mahali pa kazi (Risk assessment); 
 5. Kufanya mapitio ya michoro na majenzi ya sehemu za kazi; 
 6. Kufanya uchunguzi wa Afya na magonjwa kulingana na kazi husika mahali pa kazi; Kufanya uchunguzi wa ajali (accident investigation); 
 7. Kufanya tathmini ya athari za kimazingira (Industrial hygiene surveys and measurements) pamoja na;
 8. Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu masuala ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi.

DIRA

 • Kujenga nguvukazi salama na yenye afya njema kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu

DHIMA

 • Kusimamia, Kuwezesha, Kuelimisha na Kuhamasisha masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kuweka mifumo thabiti itakayo zuia ajali, magonjwa na vifo pamoja na uharibifu wa mali ili kupunguza gharama za uendeshaji na kukuza uchumi wa Taifa.