Kanda hii inaundwa na mikoa mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Makao makuu ya kanda hii yapo Mtwara. Wengi wa wakazi wa kanda hii ni wakulima wa korosho lakini kanda hii inajulikana pia kwa kuwa na viwango vikubwa vya gesi asilia. Shughuli zote hizi za kiuchumi zinahitaji mifumo thabiti ya kuhakikisha ufuataji wa sheria, kanuni na viwango vya usalama na afya ya watu wanaojishughulisha na shughuli hizo muhimu za kiuchumi. Shughuli nyingine zinazoendeshwa katika kanda hii ni pamoja na biashara na uzalishaji wa viwandani.